Wastara: Nisingekuwa Jasiri Ningeshakufa Siku Nyingi

STAA wa fi lamu ambaye amepitia misukosuko mingi kwenye maisha yake, Wastara Juma amefunguka kuwa kama asingekuwa mwanamke jasiri maishani mwake angekuwa amekufa siku nyingi.

Akizungumza na AMANI staa huyo alisema kuwa wanawake wengi wanapokutana na magumu maishani wanakata tamaa haraka na wengine hata kufi kia hatua ya kujitoa uhai.

“Unajua siku zote nikiangalia maisha niliyopitia kwa kweli nabaki najiuliza maswali mengi na ninajua wazi kama sio moyo wangu kubeba ujasiri ningeshaondoka kwenye dunia hii, hili liwe fundisho kwa wanawake wengine wengi,” alisema Wastara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.