CHEZEA mapenzi wewe! Mtu akipenda haoni wala haambiwi, umemsikia msanii wa vichekesho, Anna Exvery ‘Ebitoke’? Aanasema kuwa anawashangaa watu wanavyoponda mapenzi yake yake na msanii mwenzake, Yusuph Mlela. Akibonga na Za Motomoto ya Risasi, Ebitoke alisema kuwa hata kama watasema vipi yeye na Mlela wameshapendana na hakuna wakuwatenganisha hata kama wanasema hawaendani bali Mlela kafa kaoza kwake.
“Halafu kinachonishangaza wanajua mimi na Mlela tumeanza jana wakati tulianza uhusiano muda mrefu sana na maneno yao hayawezi kuvunja uhusiano wetu, kama hatujaendana wao wameendana naye? Tena watambue Mlela haoni wala hasikii yaani kafa kaoza kwangu,” alisema Ebitoke.